Mashindano ya kila mwaka ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa mbinu ya tajweed yanayojulikana kwa jila la Hilal yameanza leo Jumamosi mjini Riadh Saudi Arabia.
2010 Aug 21 , 15:14
Sherehe ya kushukuriwa na kutuzwa washindi wa mashindano ya 10 ya Qur'ani ya al-Jabir katika Umoja wa Falame za Kirabu ilifanyika siku ya Jumanne huko Abu Dhabi mji mkuu wa Imarati.
2010 Aug 19 , 11:37
Sambamba na kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani, askari usalama wa Saudi Arabia wamekuwa wakitekeleza operesheni mpya maalumu za kuvuruga na kubana shughuli za Qur'ani zinazoendeshwa na raia wa Kishia nchini humo.
2010 Aug 19 , 11:36
Mashindano ya saba ya “Zawadi ya Kimataifa ya Qiraa, Tartil na Tafsiri ya Qurani Tukufu” yatafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 26 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini Algeria.
2010 Aug 18 , 16:01
Kitengo cha kimataifa cha Maonyesho ya Qur’ani ya Tehran kitazinduliwa rasmi Jumamosi ijayo tarehe 21 Agosti, sambamba na Ramadhani kumi.
2010 Aug 18 , 12:53
Mashindano ya 14 ya Kimataifa ya Qur’ani, Zawadi ya Dubai yalianza jana katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2010 Aug 18 , 12:08
Mashindano ya Qur’ani makhsusi kwa ajili ya wanajeshi yalianza jana tarehe 17 Agosti katika mji mkuu wa Qatar Doha yakiwashirikisha washindani 60.
2010 Aug 18 , 12:04
Jumuiya ya Kiislamu ya Ghadir ya nchini Ufaransa inatekeleza ratiba maalumu kwa ajili ya Waislamu wa nchi hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
2010 Aug 18 , 12:02
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 29 na 30 za mwezi huu wa Agosti katika Msikiti Mkuu wa London ikiwa ni katika ratiba za msikiti huo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
2010 Aug 18 , 11:58
Mashindano ya kieneo ya 18 ya kuhifadhi Qur’ani ya Senegal yatafanyika Jumapili ijayo katika mji wa Tiyas.
2010 Aug 17 , 17:50
Ofisi ya Mkuu wa Jumuiya ya Misiki nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa nakala milioni moja za kitabu kitukufu cha Qur'ani zinagawanywa kwa watu wanaozuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika Masjidul Haraam ikiwa ni sehemu ya mpango wa kudhamini mahitaji ya watu wanaozuru na kutekeleza ibada ya sala katika msikiti huo.
2010 Aug 17 , 12:37
Mashindano ya 14 ya kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yameanza leo Jumanne katika mkoa wa Umran nchini Yemen.
2010 Aug 17 , 12:04
Awamu ya kwanza ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa walemavu wa akili yalianza siku ya Jumapili huko Cairo mji mkuu wa Misri.
2010 Aug 17 , 12:04