Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa nakala milioni moja za Qur’ani Tukufu zitachapishwa hapa nchini mkabala wa kila Qur’ani inayochomwa moto au kuvunjiwa heshima.
2010 Sep 14 , 18:54
Wanaharaakti wa intaneti wamepanga kukusanya saini milioni moja kupinga hatua ya kishenzi ya kuchoma Qurani Tukufu ya Wakristo wenye misimamo mikali Marekani.
2010 Sep 14 , 07:56
Wasomaji wakongwe wa Qur'ani Tukufu nchini Iran wamezungumzia maafa ya kuvunjiwa heshima kitabu kitukufu cha Qur'ani kwa kuchomwa moto nchini Marekani wakisema kuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe (SW) ndiye atakayeilinda Qur'ani Tukufu.
2010 Sep 13 , 11:11
Mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika mkoa wa Golistan nchini Iran ametoa taarifa akilaani njama za kishetani zinazohujumu Uislamu za kundi la Wakristo wenye misimamo mikali nchini Marekani na kusema kuwa serikali ya Washington na Wazayuni ndiyo wanaopaswa kulaumiwa na kubebeshwa makosa hayo makubwa.
2010 Sep 13 , 11:11
Jumuiya ya makundi ya kujitolea ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran imetoa taarifa kuhusu jinai ya kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani ikisisitiza kuwa tukio hilo litaleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwaondoa Waislamu wengi katika usingizi.
2010 Sep 13 , 11:10
Mustafa Ismail ni miongoni mwa shakhsia na makari wa Qur'ani waliokuwa na taathira kubwa katika maisha yangu ya Kiqur'ani na kiraa yake imesaidia sana katika kustawisha usomaji wangu.
2010 Sep 12 , 15:50
Baada ya Kasisi Terry Jones wa Kanisa la Dove World Outreach Center katika jimbo la Florida la Marekani kutupilia mbali mpango wake wa kuchoma moto Qur'ani katika kumbukumbu ya mashambulizi ya Septemba 11, sasa kanisa jingine la mji wa Topeka makao makuu ya jimbo la Kansas limetangaza kuwa litachoma moto kitabu hicho kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.
2010 Sep 12 , 12:55
Nakala ya tarjumi ya Qur’ani kwa lugha mbili za Kiingereza na kifaransa ilizunduliwa jana katika mji wa Ajman katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2010 Sep 09 , 12:16
Jumuiya ya Makanisa ya Kiprotestanti ya Indonesia (PGI) imelaani hatua ya kanisa la Marekani ya kutangaza tarehe 11 Septemba kuwa ni siku ya kimataifa ya kuchoma moto Qur’ani na kusema kuwa hatua hiyo itachafua uhusiano kati ya Uislamu na Ukristo.
2010 Sep 09 , 12:10
Tamasha la kwanza la Qur'ani la Washia limepangwa kufanyika leo Jumatano tarehe 8 Septemba huko katika mji wa al-Awamiyah katika mkoa wa Qatif nchini Saudi Arabia.
2010 Sep 08 , 17:53
Kituo cha Kiislamu cha Ruyigi kilifunguliwa siku ya Jumatatu katika mji wa Ruyigi nchini Burundi.
2010 Sep 08 , 17:47
Mamia ya wananchi wa Afghanistan wamemiminika mabarabarani kulalamikia kitendo cha Marekani cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu. Waandamanaji hao wametoa wito wa kulindwa Qur'ani Tukufu mbele ya mashambulizi ya maadui
2010 Sep 07 , 17:35
Tamasha la kila mwaka la kuwaenzi Mahafidhi wa Qur'ani Tukufu limefanyika nchini Misri na kuhudhuriwa na Mahafidhi 400 wa Qur'ani Tukufu.
2010 Sep 07 , 11:33