Mwandishi mashuhuri anayeandika makala katika gazeti la New York Times Nicholas Christopher amewaomba radhi Waislamu kote duniani hususan Waislamu wa nchi hiyo kutokana na kuongezeka wimbi la ubaguzi dhidi ya Waislamu na propaganda chafu dhidi ya dini hiyo nchini Marekani.
2010 Sep 20 , 17:31
Vikao vya muda mfupi vya kufasiriwa Surat al-Hujurat vitafanyika katika Kituo cha Vijana wa Kiislamu mjini Manchester (MYF) Uingereza kuanzia Jumamosi tarehe 16 0ktoba.
2010 Sep 20 , 17:13
Mashindano ya 23 ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu na hadithi kwa vijana wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi yalianza siku ya Jumapili tarehe 19 Septemba huko Sharja katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2010 Sep 20 , 17:11
Masomo maalumu ya Qur'ani kwa wanawake wa Qatar yameanza siku ya Jumamosi tarehe 18 Septemba na yamepangwa kuendelea hadi mwezi Februari mwakani.
2010 Sep 20 , 17:04
Sherehe za ufunguzi wa taasisi ya Qur’ani na Hadithi ya al Zahra (as) zimefanyika mjini Islamabad Pakistan zikihudhuriwa na hafidhi wa Qur’ani nzima Muhammad Taqi na kwa hotuba ya mkuu wa taasisi hiyo Idris Ahmad Alawi. Sherehe hizo zimehudhuriwa na mamia ya wakazi wa miji ya Islamabad na Rawalpindi.
2010 Sep 20 , 08:04
Mashindano ya 16 ya Qur’ani Tukufu ya kitaifa makhsusi kwa ajili ya vijana wa Kuwait yataanza tarehe 25 Septemba na kumalizika tarehe 30 mwezi huu.
2010 Sep 20 , 00:05
Ahmad al-Misrawi, Sheikh al-Qurra wa Misri au kwa ibara nyingine shekhe wa wasomaji Qura'ni wa Misri amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa shule za mafunzo ya Qur'ani Tukufu na kushiriki wasomaji mashuhuri wa Qur'ani katika mafunzo ya shule hizo.
2010 Sep 19 , 23:30
Mashindano ya 16 ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa vijana wa Kuwait yamepangwa kuanza Jumamosi tarehe 25 Septemba na kuendelea hadi Alkhamisi tarehe 30 Septemba.
2010 Sep 19 , 23:01
Makasisi kadhaa wa Kikristo wa Iraq wamelaani kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Marekani wakikitaja kuwa ni kinyume na mafundisho ya Kikristo.
2010 Sep 18 , 16:35
Mafunzo ya thamani za Qur'ani yatatolewa nchini Sudan tarehe 20 hadi 22 mwezi huu Septemba chini ya usimamizi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
2010 Sep 18 , 16:33
Kitendo cha baadhi ya Wakristo wenye misimamo mikali cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu ni kielelezo cha chuki na vinyongo vya maadui wa Uislamu na Qur'ani Tukufu na jibu lake linapaswa kuwa la kistaarabu na kuzingatia maadili mema.
2010 Sep 18 , 16:32
Mwakilishi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amemkosoa Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo kwa kupuuza suala la kuchomwa moto Qur’ani nchini Marekani.
2010 Sep 14 , 19:13
Waziri wa Utamaduni wa Iran:
Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa nakala milioni moja za Qur’ani Tukufu zitachapishwa hapa nchini mkabala wa kila Qur’ani inayochomwa moto au kuvunjiwa heshima.
2010 Sep 14 , 18:54