Mwanachama mmoja wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Misri amesema kuwa matamshi ya dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu yaliyotolewa na Kasisi al Anba Bishoy wa Misri yametolewa kwa uungaji mkono wa kanisa na Papa Shenouda III, Kiongozi wa Kanisa la Makopti ambaye ni maarufu kwa kuupiga vita Uislamu.
2010 Sep 29 , 15:24
Ukurasa wa nakala ya zamani ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa katika nusu ya kwanza ya karne ya kwanza Hijria katika kipindi cha utawala wa Imam Ali bin Abi Twalib (as) utauzwa tarehe 16 Oktoba mjini London.
2010 Sep 27 , 14:58
Vijana wapatao 2400 wa Kuwait wanashiriki katika duru ya 16 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani.
2010 Sep 27 , 13:20
Vipindi maalumu vya masomo kwa wahubiri wa Kiislamu na maimamu wa misikiti ya mikoa tofauti ya Misri vitaanza kutolewa tokea siku ya Jumatatu tarehe 27 Septemba katika Msikiti wa an-Nur mjini Cairo na kuendelea kwa muda wa miezi miwili.
2010 Sep 26 , 12:42
Ratiba ya washiriki wa duru ya utangulizi ya mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Afrika Kusini tayari imeainishwa na Tasisi ya Qur'ani ya Afrika Kusini na washiriki watatangaziwa ratiba hiyo hii leo Alkhamisi.
2010 Sep 23 , 12:54
Nuskha mbili adimu za Qur'ni Tukufu zinahifadhiwa katika maktaba ya Chuo cha Williams katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani. Hayo yamesemwa na Win G. Hammond mmoja wa wakuu wa chuo hicho.
2010 Sep 23 , 12:51
Kamati ya Uarifishaji Uislamu ya Kuwait imetangaza habari ya kutekelezwa mpango wa uchapishaji na kutarjumu Qur'ani Tukufu kwa lugha mbalimbali nchini humo.
2010 Sep 22 , 12:29
Kufikia sasa wasanii 250 kutoka nchi 32 za dunia wamejiandikisha kushiriki katika kuongamano la wanakaligrafia wa Qur'ani Tukufu ambalo limepangwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Madina tarehe 26 Aprili hadi 2 ya mwezi Mei mwaka ujao.
2010 Sep 21 , 17:14
Washindi wa mashindano ya Qur'ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya walemavu wa akili walienziwa na kutuzwa Jumatatu ya jana katika mji mkuu wa Misri Cairo.
2010 Sep 21 , 14:14
Mashindano ya tano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la 'Mama Kigezo' makhsusi kwa ajili ya wanawake yatafanyika tarehe 16 Oktoba katika mskiti mkuu wa Kuwait.
2010 Sep 21 , 13:58
Tukio la kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini Marekani si jambo lililoanzishwa na kasisi wa kanisa dogo tu la Marekani bali ni njama kabambe iliyopingwa tokea huko nyuma.
2010 Sep 21 , 12:20
Mashindano ya taifa ya kusoma Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 24 hadi 26 za mwezi huu wa Septemba katika mji wa Cape Town huko Afrika Kusini.
2010 Sep 20 , 17:48
Mwandishi mashuhuri anayeandika makala katika gazeti la New York Times Nicholas Christopher amewaomba radhi Waislamu kote duniani hususan Waislamu wa nchi hiyo kutokana na kuongezeka wimbi la ubaguzi dhidi ya Waislamu na propaganda chafu dhidi ya dini hiyo nchini Marekani.
2010 Sep 20 , 17:31