Masomo ya kuhifadhi na tajwidi ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake yameanza leo katika Kituo cha Qur'ani cha al Atrijah katika mji wa Ajman kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.
2010 Oct 09 , 13:48
Washindi wa mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani nchini Rwanda walienziwa na kuzawadiwa katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Kigali.
2010 Oct 06 , 18:59
Mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani ambayo yanatazamiwa kufanyika nchini Qatar chini ya anwani ya 'Familia Hafidh' na ambayo ni mashindano maalumu kwa ajili ya familia za nchi hiyo, yamepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.
2010 Oct 05 , 17:07
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali kitendo cha walowezi wa Kizayuni cha kuchoma moto msikiti wa al Anbiyaa na nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika kijiji kimoja cha mji wa Bait Laham katika Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan.
2010 Oct 05 , 15:59
Duru ya 10 ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani tukufu itafanyika katika mji wa Vancouver nchini Canada Aprili mwakani.
2010 Oct 04 , 22:28
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yamefanyika katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kwa hima ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani.
2010 Oct 04 , 19:43
Mshindano ya kimataifa ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur'ani na hadithi za Bwana Mtume (saw) yalianza jana Jumamosi huko Jakarta mji mkuu wa Indonesia.
2010 Oct 03 , 19:13
Mashindano ya kila mwaka ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yalimalizika siku ya Ijumaa huko Kuwait.
2010 Oct 03 , 19:04
Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani CAIR limeazimia kutoa zawadi ya nakala za Qur'ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kiingereza katika kongamalo lake la kila mwaka.
2010 Oct 02 , 16:19
Kitengo cha masuala ya dini na vijana cha Kituo cha Vijana cha Doha mji mkuu wa Qatar kinatayarisha masomo ya msingi ya kinadharia na kivitendo ya elimu ya tajwidi na tartili ya Qur'ani Tukufu.
2010 Oct 02 , 16:18
Ujumbe wa wasomaji Qur'ani na wahudumu wa Haram ya Imam Hussein na Hadharat Abbas (as) umekitembelea Kituo cha Qur'ani cha Hadharat Ruqiyya (as) katika mji mtakatifu wa Qum.
2010 Oct 02 , 11:47
Duru ya kwanza ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kwa wanawake wa Iraq imepangwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Kadhimein.
2010 Oct 02 , 11:35
Mwanachama mmoja wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Misri amesema kuwa matamshi ya dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu yaliyotolewa na Kasisi al Anba Bishoy wa Misri yametolewa kwa uungaji mkono wa kanisa na Papa Shenouda III, Kiongozi wa Kanisa la Makopti ambaye ni maarufu kwa kuupiga vita Uislamu.
2010 Sep 29 , 15:24