Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar imevitahadharisha viwanda vya uchapishaji Qur'ani vya Misri kwamba iwapo vitachapisha nakala za Qur'ani zenye makosa ya kiuchapishaji zitanyang'anywa kibali.
2010 Oct 20 , 18:52
Dharau ya nchi za Magharibi dhidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani imechunguzwa katika toleo jipya la 326 la jarida la Kiarabu la al-Wahda linalojadili masuala ya kidini, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.
2010 Oct 20 , 10:05
Ayatullah Seyyid Abul Qasim Dibaji, Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Fiqhi ya Kiislamu amesema uchochezi wa kimakundi ni kufri kubwa zaidi kwa mtazamo wa mafundisho ya Qur'ani.
2010 Oct 19 , 21:06
Masomo ya Qur'ani maalumu kwa wafanyakazi wa baadhi ya idara za serikali katika mji wa Nasiriyya nchini Iraq yalianza jana Jumatatu tarahe 18 Oktoba katika taasisi ya Darul Qur'an.
2010 Oct 19 , 21:02
Msahafu unaosema umezinduliwa nchini Qatar kwa hima ya Kitengo cha Utamaduni cha Taasisi ya Huduma za Kibinadamu (RAF).
2010 Oct 19 , 11:40
Mashindano ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu ya Russia yanatazamiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba katika mji wa Moscow.
2010 Oct 19 , 10:41
Kongamano la Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani na Suna za Mtume (saw) limeanza katika mji mtakatifu wa Madina likihudhuriwa na wanaharakati wa kike wa masuala ya Qur'ani.
2010 Oct 18 , 16:35
Duru ya tano ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi, kufasiri na kusoma Qur'ani Tukufu yanayojulikana kwa jina la Sheikh Ghanim bin Ali yamepangwa kufanyika hivi karibuni huko Doha, mji mkuu wa Qatar.
2010 Oct 18 , 15:58
Tamasha ya pili la kimataifa la Wiki ya Qur'ani ilifunguliwa jana katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq katika sherehe iliyohudhuriwa na wawakilishi wa Rais wa Jamhuri, Waziri Mkuu na viongozi wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo.
2010 Oct 17 , 10:54
Programu ya simu za mkononi inayoweza kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha 12 hai za dunia imezinduliwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari vya Dijitali yanayoendela mjini Tehran.
2010 Oct 17 , 10:28
Nuskha moja ya Qur'ani kongwe na ya kale imegunduliwa katika kanisa la Universalist la eneo la Medford katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani.
2010 Oct 17 , 10:12
Washindi wa mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Tanzania wametunukiwa zawadi katika mji mkuu wa nchi hiyo Dar es Salaam.
2010 Oct 17 , 10:03
Kongamano la ‘Utambuzi wa Misingi, Mafundisho na Sheria za Qur’ani na Dini ya Kiislamu’ limepangwa kufanyika tarehe 24 Oktoba katika jimbo la Illinois nchini Marekani.
2010 Oct 16 , 14:19