Qari kutoka Tanzania aliyeshiriki katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani ya Wanachuo waislamu amesema kiwango cha mashindano kilikuwa cha kuridhisha na ametoa wito kwa waandalizi kuongeza idadi ya washiriki.
2011 Feb 03 , 13:49
Masomo ya muda ya Qur'ani Tukufu yataanza kutolewa katika Akademia ya Uhakiki na Sayansi za Qur'ani (ISRA) katika mji wa Sydney nchin Autralia kwa kipindi cha wiki 30.
2011 Feb 03 , 12:06
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu makhsusi kwa wanawake wa Libya yanayofanyika chini ya anwani ya 'Ittaswimu' yalianza siku ya Jumapili tarehe 30 Januari huko Tripoli, mji mkuu wa nchi hiyo.
2011 Feb 03 , 12:06
Mkutano wa kimataifa wa Qur'ani na Dua utafanyika miezi kadhaa ijayo katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
2011 Feb 03 , 12:01
Duru ya 25 ya Mashindano ya usomaji Qur'ani yanafanyika katika jimbo la Bauchi nchini Nigeria tokea Jumapili tarehe 30 Januari.
2011 Feb 03 , 12:00
Sherehe ya kuwaenzi mahafidhi wa kike wa Qur'ani imefanyika katika Kituo cha Kuhifadhisha na Tajwidi ya Qur'ani Tukufu katika eneo la Salfit katika eneo la Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan huko Palestina.
2011 Feb 03 , 11:58
Kituo cha Sultan Qaboos cha Utamaduni wa Kiislamu (SQCIC) kimetangaza kuanza usajili wa mashindano ya 21 ya Kuhifadhi Qur'ani yanayofadhiliwa na Sultan Qaboos.
2011 Feb 01 , 12:54
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litashiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wanajeshi wa Nchi za Kiislamu yatakayofanyika Saudi Arabia.
2011 Feb 01 , 12:50
Masomo maalumu ya wanawake ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yameanza katika Kituo cha Hifdhi ya Qur'ani cha az-Zahra katika mtaa wa al-Ma'mura mjini Doha.
2011 Feb 01 , 12:44
Tarjumi za Qur'ani Tukufu kwa lugha 113 tofauti za Ulaya zinahifadhiwa katika maktaba ya Mfalme Abdul Aziz mjini Riyadh, Saudi Arabia.
2011 Jan 31 , 18:33
Kanali ya televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa asilimia 90 na nakala za kitabu kitukufu cha Qur'ani katika nchi kubwa zaidi ya Kiislamu yaani Indonesia, zinachapishwa na taasisi za uchapishaji zisizokuwa za Kiislamu, suala ambalo linasababisha makosa ya kichapa.
2011 Jan 31 , 18:32
Abdalla al-Mubarak, mkuu anayesimamia masuala ya Qur'ani Tukufu na utafiti wa Kiislamu katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait ametangaza habari ya kufunguliwa kituo cha Qur'ani cha al-Wiqayan nchini humo mwezi Machi mwaka huu.
2011 Jan 31 , 13:48
Taasisi ya Dar al-Qur'an ya Qatar inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo imeanzisha mafunzo ya Qur'ani Tukufu kupitia mtandao katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha kwa ushirikiano wa Shirika la Mji wa Eletroniki la nchi za Kiarabu.
2011 Jan 30 , 16:57