Utumiaji wa sanaa plastiki (plastic arts) katika nyanja za Qur'ani unastawi kwa kasi nchini Ivory Coast. Taarifa zinasema kuwa wasaani wengi wa nchi hiyo wamekuwa wakiandika hati nzuri za aya au sura za Qur'ani Tukufu juu ya vitu wanavyobuni.
2010 Aug 12 , 15:45
Jumuiya ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Sihat nchini Saudi Arabia itaandaa kikao cha kuchunguza muundo na kalibu jumla ya sura za Qur'ani Tukufu.
2010 Aug 12 , 13:27
Awamu ya mwisho ya duru ya tano ya mashindano ya Qur'ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yatafanyika katika mji wa Sharja Umoja wa Falme za Kiarabu.
2010 Aug 11 , 11:09
Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyya kilichoko katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran kinatumia walimu wa kieneo kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu katika nchi ya Nigeria, suala ambalo limetajwa kuwa na mafanikio makubwa.
2010 Aug 11 , 11:08
Qur'ani ya dhahabu iliyoandikwa kwa mujibu wa nakala ya Othman Twaha itaonyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kaligrafia yatakayofanyika katika mji wa Velikiy Novgorod nchini Russia kuanzia tarehe 10 hadi 12 mwezi Septemba mwaka huu.
2010 Aug 10 , 15:43
Toleo la kwanza la jarida la masuala ya Qur'ani linaloandikwa na wanafunzi wa Ivory Coast wanaosoma katika Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyya katika mji mtakatifu wa Qum limechapishwa.
2010 Aug 10 , 15:41
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika katika Visiwa vya Comoro mwezi wa Muharram. Hayo ni kwa mujibu wa Muhyiddin Abdullah Mohammad Mkuu wa chumba cha Comoro katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika Tehran.
2010 Aug 09 , 17:47
Kipindi maalumu cha 'Usiku za Ramadhani' kitaanza kutangazwa katika Redio Qur'ani ya Saudi Arabia katika siku zote za mwezi huo mtukufu.
2010 Aug 09 , 10:39
Vikao vya Mwanadamu Katika Qur'ani vitafanyika mjini London, Uingereza katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2010 Aug 08 , 16:10
Nakala za kitabu kitukufu cha Qur'ani zilizotarjumiwa kwa lugha za Kifaransa, Kihispania na Kitamazight (lugha ya Mabarbari wa kaskazini mwa Afrika) zimesambazwa katika misikiti, vituo vya kuhifadhisha Qur'ani ma jumuiya za masuala ya kheri na utamaduni za Algeria.
2010 Aug 08 , 16:08
Awamu ya mwisho ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu makhsusi kwa wanawake imefanyika katika mji wa Bursa nchini Uturuki.
2010 Aug 08 , 16:06
Maonyesho ya 18 ya Kimatiafa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yanafunguliwa rasmi leo Jumamosi katika ukumbi wa sala wa Imam Khomeini.
2010 Aug 07 , 12:48
Maafisa wanaosimamia mashindano ya 14 ya kimataifa ya Qur’ani ya Dubai wametangaza ratiba ya masuala ya kiutamaduni yatakayoandamana na mashindano hayo.
2010 Aug 07 , 11:19