Idara ya Kijamii, Kujitolea na Kibinadamu, inayohusishwa na Urais wa Misikiti Miwili Mitakatifu, imetangaza leo kwamba karibu waumini milioni 30 wamefaidika na huduma za kujitolea katika Msikiti Mtakatifu Mkuu tangu kuanzishwa mwaka jana hadi robo ya kwanza ya mwaka huu wa 1444 Hijria Qamaria.
Kwa mfano, kulingana na takwimu za hivi punde, milo ya kufugua saumu au futari imetolewa kwa waumini 5,915,193. Aidha chupa 2,357,190 za maji yenye baraka ya Zamzam zimekabidhiwa waumini katika eneo hilo takatifu.
Jumla ya muda wa kujitolea umefikia saa 1,213,540 zilizoongezwa na mamlaka 35 za kujitolea, zinazoshughulikia nyanja 17, na kunufaisha jumla ya waumini 29,597,552, kulingana na takwimu.
3481571