Kundi la kiutamaduni la al-Fatimiyaat la mjini al-Awamiya katika mkoa wenye wakazi wengi wa Kishia wa Qatif limeandaa tamasha la Sera za Mtume (saw) maalumu kwa wanawake wa Kishia wa Saudi Arabia kwa mnasaba wa kusherehekea Maulidi ya Mtume Mtukufu (saw).
2011 Feb 16 , 16:05
Shughuli za ujenzi wa msikiti mpya wa Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu zilizinduliwa hapo jana Jumanne na Swagr bin Muhammad al-Qasimi, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Wakfu ya Sharjah.
2011 Feb 16 , 16:02
Kituo cha Kiislamu cha mji wa Boulder katika jimbo la Colorado nchini Marekani kimeanza kuchangisha fedha za kujenga kituo kipya cha utamaduni cha Kiislamu.
2011 Feb 16 , 15:58
Waislamu wa Ethiopia walisherehekea siku ya kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) hapo jana Jumanne kwa mujibu wa riwaya ya Kisuni.
2011 Feb 16 , 15:46
Kongamano la kila mwaka la kidini na kiutamaduni la 'Machipuo ya Ujumbe' litafanyika tarehe 21 hadi 23 huko katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq kwa mnasaba wa kuadhimishwa Maulidi ya Mtume Mtukufu (saw).
2011 Feb 15 , 16:54
Idara inayosimamia Msikiti wa Rasul al-A'dham katika mji wa Kishia wa Saihat nchini Saudi Arabia imesema kuwa ujenzi wa msikiti huo umekamilika na kwamba utafunguliwa tarere 21 Februari ambayo ni siku ya kuadhimishwa Maulidi na kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw).
2011 Feb 15 , 16:29
Jumba la makumbusho la Bamoun Royal Palace katika mji wa Foumban nchini Cameroon limepanga kuonyesha faharasa ya nakala za maandishi ya Kiislamu na Kiarabu zinazohifadhiwa katika jumba hilo.
2011 Feb 12 , 13:20
Chuo Kikuu cha Muhammad bin Abdullah cha Morocco kimepanga kuitisha kongamano la kimataifa la kuchunguza maisha na sira ya Mtume Muhammad (saw) katika maandiko ya Uholanzi. Kongamano hilo limepangwa kufanyika kwa kipindi cha siku tatu katika mji wa Fas yapata miezi miwili ijayo.
2011 Feb 12 , 12:52
Akademia ya al Daawa ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu (IIU) nchini Pakistan itakuwa na sherehe za siku tano za kuadhimisha Maulidi ya Mtume Muhammad (saw) katika mwezi wa Rabiul Awwal.
2011 Feb 09 , 10:52
Insiklopedia mpya ya historia ya Uislamu ambayo ina umuhimu mkubwa katika uchunguzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu imezinduliwa katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.
2011 Feb 07 , 17:23
Wizara ya Utamaduni ya Algeria imetangaza kuwa ufunguzi rasmi wa sherehe za kuchaguliwa mji wa Tlemcen kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu zitafanyika tarehe 17 Aprili zikihudhuriwa na wawakilishi wa zaidi ya nchi 40.
2011 Feb 07 , 01:26
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limetangaza kuwa litatoa msaada wa kifedha kusaidia Kamisheni ya Taifa ya Elimu na Utamaduni ya Iraq katika mpango wake wa kustawisha elimu uliopewa jina la Nuorul Maarif makhsusi kwa watoto wa kike.
2011 Feb 01 , 18:13
Kwa mnasaba wa sherehe za Alfajiri 10 za kuadhimisha Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran maonyesho ya Qur'ani yenye anwani ya "Alfajiri ya Mapinduzi ya Kiislamu" yamefanyika katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia.
2011 Feb 01 , 12:41