Mwenyekiti wa Kamati inayoandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai Ibrahim Muhammad Bumalha amesema kuwa nchi 82 zimethitisha kwamba zitashiriki katika mashindano hayo.
2011 Jul 20 , 21:04
Mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq leo tarehe 20 Julai utafukizwa kwa marashi ya Qur'ani Tukufu kutokana na kiraa za wasomaji Qur'ani wa Kimataifa waliokwenda Iraq kwa mnasaba wa kusherehekea mpango wa kuchaguliwa Najaf kuwa mji mkuu wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka 2012.
2011 Jul 20 , 14:09
Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, imezindua kitabu maalumu chenye anwani ya " Mwezi Upi Sahihi, wa ‘kitaifa’ au ‘kimataifa’" katika kuanza na kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Jul 20 , 12:48
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia Hamid Ridha Abbasi meng'ara katika siku ya tatu ya mashindano hayo yanayofanyika mjini Kuala Lumpur.
2011 Jul 19 , 15:44
Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA lenye makao yake nchini Iran limeandaa warsha itakayojadili maudhui ya “Msikiti na Tafsiri ya Qur’ani”. Warsha hiyo itafanyika Julai 20 katika makao makuu ya IQNA mjini Tehran.
2011 Jul 19 , 13:13
Kuanzia mwaka ujao wa masomo, shule zote za sekondari za Iran zitaanza klasi kwa somo la Qur’ani la dakika tano.
2011 Jul 19 , 13:10
Mashindano ya tano ya Qur’ani ya wanawake wa mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran yatafanyika Julai 21 na 23.
2011 Jul 19 , 13:08
Darul Qur'an al Karim inayofungamana na Taasisi ya Haram ya Imam Hussein AS imetangaza kuwa itaandaa vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
2011 Jul 18 , 16:54
Mkurugenzi wa kitengo cha teknolojia ya dijitali katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran amesema kazi 20,000 za dijitali zitawasilishwa katika maonyesho hayo.
2011 Jul 18 , 16:46
Mashindano ya 9 ya kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yanafanyika katika mji mtakatifu wa Madina yakiwashirikisha wanafunzi 350 kutoka nchi 25 duniani.
2011 Jul 16 , 15:34
Awamu ya 15 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Kuwait itafanyika mwezi Oktoba, imetangaza Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu nchini humo.
2011 Jul 14 , 09:12
Mkuu wa Jumuiya ya Wasomaji na Wanaohifadhi Qur'ani katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq amesema mji huo utakuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani mwakani.
2011 Jul 14 , 09:07
Mashindano ya 53 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yatafunguliwa rasmi Jumamosi ijayo katika sherehe itakayohudhuriwa na mfalme na nchi hiyo na mke wake katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
2011 Jul 13 , 18:12