IQNA

Waislamu Marekani

Jela ya Kentucky Marekani kuruhusu Hijabu baada ya mapatano

17:31 - April 19, 2024
Habari ID: 3478701
IQNA - Mapatano yamefikiwa katika kesi inayohusu jela ya Mkoa wa Warren iliyoko Bowling Green, Kentucky, nchini Marekani kuhusu mwanamke Muislamu kunyimwa haki yake ya kidini ya kuvaa Hijabu.

Jela ilikuwa imemlazimisha kuvua hijabu yake, kupiga picha  na kuiweka katika mtandao wa jela bila idhini yake.

Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu (CAIR)shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani, lilitangaza kusuluhishwa kwa kesi hiyo.

CAIR iliwasilisha kesi hiyo mwaka jana kwa lengo la kutaka picha hiyo iharibiwe. Mteja ambaye jina lake rasmi halikutajwa na ametambuliwa kama Jane Doe ili kulinda utambulisho wake.

Baada ya kuwasilishwa kwa kesi hiyo, jela ya Mkoa wa Warren County (WCRJ) ilichukua hatua za haraka kuondoa picha ya Bi. Doe kwenye hifadhidata ya jela na hivyo haipatikani tena katika mitandao ya taasisi za kiserikali.

Kwa mujibu wa mapatano  kati ya CAIR na Jela ya Mkoa ya Warren County (WCRJ), jela imeahidi in kuheshimu imani ya wafungwa wa kidini na inabadilisha sera yake ili kuakisi hilo.

Kuanzia sasa, watu waliopigwa picha hawatahitajika kuondoa mitandio au Hijabu wakati wa kupigwa picha. Mabadiliko ya sera pia yatajumuisha marekebisho mengine madogo ambayo yanahakikisha kuwa haki za kidini za wafungwa zinazingatiwa.

 "Huu ni ushindi kwa jumuiya ya kidini ya Warren County kwa ujumla. Mteja wetu anafurahi kujua kwamba, sio tu kwamba picha yake akiwa hana Hijabu imeondolewa, lakini hakuna mtu mwingine atakayestahimili kile alichofanyiwa, "alisema Mwanasheria wa CAIR Aya Beydoun. "Tunashukuru sana Jela ya Mkoa wa Warren kwa kufanya kazi nasi kufanya mabadiliko haya."

3487988

captcha