IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 92

Surah Al-Layl inazungumza kuhusu wanaotoa fedha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu

17:30 - July 05, 2023
Habari ID: 3477244
TEHRAN (IQNA) – Linapokuja suala la fedha na mali, watu wamegawanyika katika makundi mawili: wale wanaotumia fedha zao kusaidia wengine na wale wanaojilimbikizia mali bila ya kuwasaidia wengine.

Vikundi vyote viwili vitakumbana na kifo na wala hawatachukua pesa zao kwenda kwenye ulimwengu ujao, kulingana na Surah Al-Layl.

Al-Layl ni sura ya 92 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 21 na iko katika Juzuu ya 30. Ni Makki na ni Sura ya 9 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Neno Layl (usiku) limetajwa mara 92 ndani ya Qur'ani Tukufu, ikiwa ni pamoja na katika aya ya kwanza ya Surah Al-Layl, ambayo imeipa jina lake.

Sura hii inazungumzia makundi mawili ya watu: Wale wachamungu na wakarimu na wale wanaofanya ubakhili.

Wale walio katika kundi la kwanza wanatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wanatoa pesa zao ili kupata radhi ya Mwenyezi Mungu na kutakasa nafsi zao. Qur'ani Tukufu inawaahidi kuridhika na wokovu na furaha ya Mwenyezi Mungu.

Wale wa kundi la pili wana mioyo chafu. Wao ni wabakhili na wanaona kesho akhera na Janna kuwa uongo. Qur'ani Tukufu inatishia kundi hili kukabiliwa na maangamizi.

Sura inasema watu hawa hawasaidii wengine kutokana na ubakhili wao bali wajue kuwa mali zao hazitakuwa na manufaa kwao baada ya kufa na Siku ya Kiyama.

Sura inataka kuwaonya na kuwasaidia watu kuelewa matokeo ya juhudi zao yatakuwaje. Inasema kwamba wengine hukubali  ahadi za Mwenyezi Mungu ambaye naye huwapa uzima wa milele uliojaa furaha. Wengine ni wabakhili, wanajiona kuwa huru na kukataa ahadi za Mungu. Ndio maana wanasonga kuelekea uharibifu.

Katika kufasiri Aya ya 12 ya Surah Al-Layl, “Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu," Allamah Tabatabai anasema katika Tafisiri ya Al-Mizan ya Qur’ani Tukufu kwamba uwongofu wakati mwingine unahusu kuonyesha njia na wakati mwingine maana yake ni kumpeleka mtu ambaye anatafuta mwongozo popote anapotaka kwenda. Mwongozo katika aya hii unaweza kumaanisha nukta ya kwanza na ya pili.

Ikiwa jambo la kwanza ndilo, basi inamaanisha kuwaongoza watu kuelekea kumwabudu Mungu, ambalo ndilo lengo la kuwaumba wanadamu. Na katika hali ya pili, inamaanisha kuwaongoza watu kwenye maisha safi, Janna  na wokovu wa milele.

captcha