Mkuu wa Kamati ya Kimataifa katika Gholam Reza Noui amesema kuwa Maoneysho ya 24 ya Kimataifa ya Qur'ani
Tukufu mjini Tehran yana washiriki kutoka nchi 20 za kigeni ikiwa ni
pamoja na nchi kadhaa za Ulaya, Afrika Kaskazini na nchi za Kiislamu
zinazopakana na Iran.
Ameongeza kuwa, kuna wataalamu wa Qur'ani kutoka nchini 15 wanaoshiriki katika maonyesho ya mwaka huu.
Kati ya nchi za kigeni zinazoshiriki maonyesho ya mwaka huu ni Algeria, Uturuki, Iraq na Italia.
Maonyesho ya mwaka huu ambayo yalianza tarehe Mosi mwezi Mtukfuu wa
Ramadhani na kufunguliwa rasmi tarehe 13 Juni yanatazamiwa kumalizika 30
Juni. Maonyesho hayo yana vibanda 300 huku kitengo cha vitabu kikiwa
kikubwa zaidi.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran ni makubwa zaidi ya aina yake duniani.
Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran, Tehran ambapo huwa na vitengo kadhaa vya maudhui mbali
mbali za Qur'ani.