IQNA

Kikao cha wasomi wafasiri wa Qur’ani chaanza Qum, Iran

12:12 - November 18, 2015
Habari ID: 3454168
Kikao cha 12 cha wasomi wafasiri wa Qur’ani Tukufu kimeanza Jumanne hii katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.

Kikao cha 12 cha wasomi wafasiri wa Qur’ani Tukufu kimeanza Jumanne hii katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
Mkutano huo umefanyika kwa mnasaba wa mwaka wa 35 wa kumbukumbu ya kuaga dunia mfasiri mashuhuri wa Qur’ani Allamah Tabatabai katika nyumba ya mwanazuoni huyo ambaye pia alikuwa mwanafalsafa.
Wafasiri na wasomi 400 wa Qur’ani kutoka kote Iran wanashiriki katika kikao hicho cha siku tatu.
Kati ya wanazuoni wa ngazi za juu wanaotazamiwa kuhutubu katika kikao hicho ni Ayatullah Abdullah Javad Amoli, Ayatullah Mohammad Yazdi na Ayatullah Jafar  Sobhani.
Allamah Muhammad Hussein Tabatabai  alifariki Novemba 1981 akiwa na umri wa miaka 80. Mwanazuoni huyo mkubwa alizaliwa katika mji wa Tabriz, kaskazini magharibi mwa Iran. Msomi huyo wa Kiislamu alikuwa hodari sana katika elimu za falsafa, irfani, tafsiri ya Qur’ani na vilevile katika masuala ya fasihi, hisabati na fiqihi. Allamah Tabatabai ameandika vitabu vingi na miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni tafsiri ya Qur'ani ya al-Mizan.

3454073

captcha