IQNA

Kikao cha Kuttadabari Qur'ani kufanyika Uingereza

14:46 - November 15, 2015
Habari ID: 3452856
Kikao cha Nne cha Kimatiafa cha 'Masomo ya Qur'ani na Kutadabari Qur'ani Tukufu Ulaya" kitafanyika Julai mwaka 2016 Manchester Uingereza.

Kwa mujibu wa tovuti ya tafsir.net, kikao hicho kimeandaliwa na Akademia ya Masomi ya Qur'ani Ulaya kwa ushirikiano wa 'Jumuiya ya Tebyan ya Qur'ani Tukufu na Masomo ya Qur'ani.'
"Uadilifu na Urehemuzu wa Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume SAW" ni anuani ya kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Kituo cha Turathi za Kiislamu mjini Manchester.
Kuarifisha Qur'ani Tukufu, kusisitiza kuhusu ulazima wa kutadabari Qur'ani Tukufu na kustawisha masomo na utafiti wa kitabu hicho kitakatifu ni kati ya malengo ya kikao hicho.
Halikadhalika kikao hicho cha kimataifa kitalenga kufasiri aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume SAW.
Kati ya malengo mengine ya kikao hicho ni kubainisha kuhusu utukufu na ujumbe wa kimataifa wa Uislamu na kubainisha namna dini hii inavyotetea uadilifu wa kijamii sambamba na kubainisha kuhusu sheria za Kiislamu na pia kuarifisha miujiza ya Qur'ani.

3447954

captcha