IQNA

IQNA yapata zawadi katika maoneysho ya vyombo vya habari

15:04 - November 14, 2015
Habari ID: 3449242
Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA) imepata zawadi ya shirika bora la habari za kidini katika Maonyesho ya 21 ya Habari na Mashirika ya Habari mjini Tehran.

Mkurugenzi wa IQNA, Hamid Saber Farzam alipokoa cheti cha heshima kwa mnasaba wa ushindi huo katika hafla iliyofanyika Ijumaa jioni mjini Tehran.
Maonyesho ya 21 ya Habari na Mashirika ya Habari yalifunguliwa rasmi Jumapili iliyopita mjini Tehran katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Hassan Rouhani.
Maonyesho hayo yalishiriksha vyombo 700 vya habari vya kitaifa. Aidha kuna washiriki kutoka Ujerumani, Italia, Marekani, China , Ufaransa, Uturuki, Kuwait, Lebanon, Japan, Iraq na Russia. Maonyesho hayo yanaendelea hadi Novemba 13 chini ya kauli mbiu ya 'Ukosoaji wa kiadilifu na uwajibikaji."

3447678

captcha