IQNA

Vijana wa Kishia watia fora mashindano ya Qur'ani Saudia

11:46 - November 10, 2015
Habari ID: 3446588
Vijana wanne wa Kishia nchini Saudi Arabia wamefanikiwa kuchukua nafasi za juu katika awamu ya tatu wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani na Hadithi yaliyofanyika katika mji mtakatifu wa Madina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA akinukulu Shirika la Habari la Qaq, wanafunzi waliopata nafasi za juu ni kutoka Taasisi ya Qur'ani ya Tarteel Al Fajr inayosimamiwa na Kituo cha Utamaduni wa Alam al Hudaa huko Safwa katika eneo la Qatif Saudi Arabia.
Seyyed Abdullah Rami Hashim Al-Sadah na Abdullah Ahmad Al Mubarak walipata nafasi za nne na sita kwa taratibu katika mashindano ya kuhifadhi Juzuu tano za Qur'ani.
Katika huhifadhi Juzuu 20 za Qur'ani Seyyed Muhammad Hashim Al-Shuraf alipata nafasi ya saba na Tahir Fathi Al Abdulla alipata nafasi ya 13 katika kuhifadhi Juzuu 13.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa wanafunzi wa taasisi hiyo ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia Saudia kupata nafasi za juu katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani nchini humo.

3444816

captcha