IQNA

Mtoto wa miaka 9 Msomali katika mashindano ya Qur'ani Saudia

18:52 - November 09, 2015
Habari ID: 3446375
Abdulswamad bin Omar Muhammad kutoka Somalia ndie mshiriki mwenye umri mdogo zaidi katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Msomali huyo mwenye umri wa miaka tisa anashiriki katika mashindano ya 37 ya kimataifa ya Qur'ani nchini Saudia. Amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na ameonyesha umahiri wa hali ya juu katika usomaji wa Qur'ani kwa kuzingatia kanuni zote mbali na kuwa na sauti na lahni nzuri.
Abdulswamad bin Omar Muhammad amesema amebainisha furaha yake kushirikia katika mashindano hayo ya Qur'ani yanayofanyika katika mji Mtakatifu wa Makka ndani ya Masjidul Haram. Amesema amefurahi zaidi kwani ndio mara ya kwanza anapata furasa ya kuizuri Nyumba ya Allah SWT na kuuona mji wa Makka al-Mukarama kwa karibu.
Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Saudia yalianza tarehe 7 Novemba na yameandaliwa na wizara ya Awqaf ya nchi hiyo. Mashindano hayo yanajumuisha washiriki 124 wasomaji na waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi 66.

3444804

captcha