IQNA

Rais Rouhani wa Iran

Mimi huanza siku yangu kwa kusoma Qur'ani Tukufu

14:08 - November 08, 2015
Habari ID: 3444795
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja Qur'ani Tukufu kuwa ni kitabu cha nuru na uongozi na kuongeza kuwa yeye daima huanza siku yake kwa kusoma kurasa kadhaa za kitabu hicho kitakatifu.

Akizungumza Jumapili wakati alipotembelea  kibanda cha Shirika la Kimatiafa la Habari za Qur'ani IQNA, katika  Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari mjini Tehran, Rais Rouhani amesema Qur'ani Tukufu humuonyesha kila mtu njia ya nuru na uono wa mbali.
Amesisitiza kuwa Qur'ani Tukufu ni rasilimali kubwa zaidi ya kimaanawi, kisheria na kisiasa sambamba na kuwa chanzo cha umoja wa Waislamu.


"Qur'ni ni rehema, tiba na muongozo hata kwa wasiokuwa Waislamu", amesema rais Rouhani.
Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari yamefunguliwa rasmi mapema leo asubuhi. Maonyesho hayo yanashiriksha vyombo 700 vya habari vya kitaifa. Aidha kuna washiriki kutoka Ujerumani, Italia, Marekani, China , Ufaransa, Uturuki, Kuwait, Lebanon, Japan, Iraq na Russia. Maonyesho hayo yanaendelea hadi Novemba 13 chini ya kauli mbiu ya 'Ukosoaji wa kiadilifu na uwajibikaji.".../mh

3444574

captcha