IQNA

Mafanikio ya Imam Khomeini MA yalitokana na Qur'ani

13:12 - November 01, 2015
Habari ID: 3428213
Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran Ayatullah Hashemi Rafsanjani amesema kuwa Qur'ani tukufu ilikuwa chanzo cha shakhsia na mafanikio makubwa ya hayati mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA.

Ayatullah Rafsanjani ameyasema hay oleo mjini Tehran alipohutubu katika kongamano la kimataifa la "Qur’ani Katika Sirah na Fikra za Imam Khomeini MA".
Ayatullah Rafsanjani ameongeza kuwa, kadiri muda unavyosonga mbele ndivyo inavyozidi kubainika namna Qur'ani Tukufu ilivyokuwa na nafasi ya kipekee katika fikra za Imam Khomeini MA.
Katika wakati ambao hakuna yeyote angeweza kuamini inawezekana, Imam Khomeini MA aliweza kuyaongoza Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hadi kupata ushindi.
Ayatullah Rafsanjani amebainisha kuwa, Imam Khomeini MA alisisitiza kuhusu umoja wa Kiislamu kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani.
Kongamano hilo la siku moja limefanyika katika Ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran ambapo wameshiriki wasomi, wanazuoni na wanafikra kutoka nchi mbali mbali duniani.
Kongamano hilo limejadili maudhui kama vile, ‘Umuhimu wa Qur’ani kwa Mtazamo wa Imam Khomeini MA,’ ‘Misingi ya Tafsiri ya Qur’ani Kwa Mtazamo wa Imam Khomeini  MA’, ‘Dhihirisho la Mafundisho ya Qur’ani Katika Mafundisho ya Kisiasa na Sirah ya Kijamii ya Imam Khomeini MA’ na ‘Maadili ya Qur’ani Katika Vitendo na Maneno ya Imam Khomeini MA.’

3427108

captcha