IQNA

Aplikesheni za kusoma Qur’ani Zapata umashuhuri

11:45 - November 01, 2015
Habari ID: 3428150
Aplikesheni za kusoma Qur’ani Tukufu zinaendelea kupata umashuhuri katika nchi za Kiislamu na hata nchi zisizokuwa za Kiislamu kote duniani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hivi sasa kuna idadi kubwa ya watu ambao huisoma Qur’ani Tukufu kwa njia ya simuerevu  za mkononi (smartphone) au tablet.
Aidha aplikesheni nyingi zina uwezo wa kuwajuza watumizi kuhusu nyakati za swala kwa njia ya adhana mbali na kuonyesha upande wa qibla popote pale alipo mtumizi.
Muslim Pro ni moja ya apilkesheni mashuhuri zaidi za Qur’ani. Aplikesheni hiyo ilitayarishwa na shirika la Bitsmedia lenye makao yake nchini Singapore na inaaminika kuwa na watumizi zaidi ya milioni 20 duniani.
Aplikesheni hiyo huwaruhusu Waislamu kudownload au kupakua Qur’ani bila malipo na huonyesha nyakati za sana na qibla.
Magdy Abdulrahman, mfanya biashara mwenye umri wa miaka 53 mjini Cairo, Misri anasema yeye husoma Qur’ani tukufu kupitia simu yake ya mkononi aina ya smartphone. Alianza kutumia aplikesheni hiyo miaka miwili iliyopita baada ya kupendekezwa na jamaa yake. Anasema aplikesheni hiyo inamfaa sana kwani anaweza kuisoma Qur’ani wakati wa faragha na kwamba pia anaweza kuyafanya maandishi yawe makubwa kutokana na udhaifu wa macho yake. Anawashukuru sana waliotengeneza aplikesheni hiyo.
Mohammad Rayan, mkaazi wa Cairo mwenye umri wa miaka 31 yeye pia anasema alianza kutumia aplikesheni hiyo mwaka 2010. Na anafurahi kuwa aplikesheni hiyo mbali na Kiarabu pia ina lugha kama vile Kiingereza, Kifaransa na Kituruki.
Imependekezwa kuwa aplikesheni kama hizo zitumike kueneza mafundisho ya Kiislamu hasa kwa kuwalenga wasiokuwa Waislamu ambao wana hamu ya kuujua Uislamu na Qur’ani Tukufu.../

3416479

captcha