IQNA

Mkutano wa Pili wa 'Kutafakari Qur'ani' waanza Morocco

16:20 - October 29, 2015
Habari ID: 3410361
Mkutano wa pili la kimataifa la kutafakari katika Qur’ani umefanyika nchini Morocco. .

Mkutano huo ulioanza Jumatani umeleta pamoja karibu shakhsia 400 wa kielimu, wahadhiri wa vyuo vikuu, wahubiri na wataalamu wa masuala ya Qur’ani Tukufu kutoka nchi tofauti za Kiarabu na Kiislamu. Washiriki wanajadili misingi ya maarifa katika kutafakari juu ya Qur’ani na kutumia njia na nyendo za shakhsia wakubwa wa karne zilizopita katika uwanja huo wa kutafakari katika kitabu hicho cha mbinguni. Aidha katika kikao hicho kinatajwa kuwa fursa chanya kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano na miamala zaidi kuhusiana na Qur’ani, kutaonyeshwa vitabu vikubwa vilivyoandikwa na shakhsia watajika wa kielimu katika uga wa taaluma ya Qur’ani Tukufu. Kuarifishwa shakhsia wakubwa katika uwanja wa kutafakari juu ya kitabu hicho, miongoni mwa watu wa zamani na wa sasa, kuimarishwa njia zinazotumika katika kutafakari aya za Mwenyezi Mungu na kuchambua nadharia za vitabu mbalimbali na kuziambatanisha na kitabu hicho cha Allah, ni miongoni mwa mambo yatakayotekelezwa na washiriki wa kongamano hilo.

3404945

captcha