IQNA

Kongamano la Utafiti wa Qur’ani kufanyika London

14:13 - October 29, 2015
Habari ID: 3409346
Kongamano la Sita la Kimataifa la Utafiti wa Qur’ani litafanyika London, Uingereza mwezi Juni mwakani.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Qur’ani litajadili madudhui ambazo zinahusi masuala ya kisasa.
Kwa mujibu wa tovuti ya  taasisi hiyo, kati ya maudhui zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na:
• Kuibuka serikali za Kiislamu na namna zinavyofuata miongozo ya Qur’ani.
• Sheria ya Qur’ani na maingiliano yake na sheria za kisekula na za kimataifa.
• Mfumo wa banki na masoko ya Kiislamu; misingi yake ya Kiislamu na tathmiini kuhusu mifumo ya sasa Kiislamu.
• Majibu ya Qur’ani kwa changamoto cha kiakademia na kifilosofia ambazo Waislamu wanakumbana nazo katika kukabiliana na fikra za wasioamini Mungu na idiolojia zinginezo.
• Misingi ya Qur’ani kuhusu harakati za kisufi au kiirfani ndani na nje ya ulimwengu wa Kiislamu.
• Namna vyombo vya habari vinavyoakisi maudhui za Qur’ani.
• Uchambuzi kuhusu taathira ya Qur’ani katika ulimwengu wa elimu, siasa, jamii saikolojia n.k
• Utafiti uliofanyika kuhusu kufahamu tafsiri za kale za Qur’ani Tukufu
• Kiarabu cha Qur’ani, je kinadorora au kinaimarika kufuatia kuibuka teknolojia mpya za habari na mawasiliano?
Hizo ni baadhi ya mada zitakazojadiliwa katika kongamano hilo na wanaotaka kushirikia wanatakiwa kupata maelezo zaidi katika tovuti iliyopo hapa chini.
http://quran-institute.org.uk

3395205

captcha