IQNA

Mazungumzo baina ya dini

Ayatullah Sistani wa Iraq asisitiza kuheshimiana miongoni mwa wafuasi wa dini mbali mbali

22:53 - December 08, 2022
Habari ID: 3476219
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq Ayatullah Ali al-Sistani amsisitiza haja ya kuzingatiwa maadili ya mshikamano unaotilia mkazo kuheshimiana miongoni mwa wafuasi wa imani au dini mbali mbali.

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu aliyasema hayo katika mkutano wa Jumatano na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa ulioongozwa na Miguel Angel Moratinos, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkuu wa Muungano wa Umoja wa Mataifa wa Staarabu (UNAOC).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Ayatullah Sistani, katika mkutano huo alisisitiza umuhimu wa juhudi za uratibu za kukuza utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani, kukataa ghasia na chuki, na kuzingatiwa kwa maadili ya mshikamano kwa kuzingatia haki na kuheshimiana miongoni mwa wafuasi wa imani tofauti.

Ayatullah Sistani aidha amesema majanga ambayo mataifa mengi na makundi ya kikabila na kijamii yanakumbana nayo katika maeneo mengi ya dunia na yanatokana na dhulma na ukosefu wa uadilifu wa kijamii na yana nafasi kubwa katika kuibuka baadhi ya makundi yenye misimamo mikali yanayotumia mabavu  dhidi ya raia wasio na ulinzi. .

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mwanazuoni huyo wa ngazi za juu alisisitiza ulazima wa kushughulikia chanzo cha matukio ya misimamo mikali na kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha haki na amani katika jamii.

Aidha Ayatullah Sistani pia alishukuru juhudi za Umoja wa Mataifa katika suala hili.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq na Muungano wa Ustaarabu pia ulitoa taarifa ya pamoja kuhusu ziara hiyo siku ya Jumatano, ambayo ilisemaa:

"Tukikumbuka mkutano kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Mwadhama (Ayatullah Sistani) tarehe 6 Machi 2021, Mwakilishi Mkuu wa UNAOC na Mwadhama walibadilishana mawazo juu ya umuhimu wa mazungumzo ya kidini na ya kidini, ambayo yamo katika msingi wa mamlaka ya UNAOC.

Moratinos alimkabidhi Ayatullah Sistani ‘mpango wa utekelezaji’ wa Umoja wa Mataifa ambao ulibuniwa mwaka wa 2019 ili kupunguza itikadi kali na kulinda maeneo ya ibada dhidi ya mashambulizi ya itikadi kali.

Mpango wa Utekelezaji wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Maeneo ya Kidini uliwasilishwa kwa Imamu Mkuu wa Al Azhar, Dkt Ahmed Al Tayeb, na Papa Francis mjini Vatican, mwaka wa 2019.

Mpango wa Utekelezaji ni wito wa kimataifa wa kuunga kanuni za msingi za ubinadamu, huruma na uvumilivu.

Bw Moratinos alisema ripoti hiyo iliandikwa ‘baada ya mashambulizi ya msikiti katika mji wa Christchurch huko New Zealand’.

"Katika Iraq pia, waumini na maeneo matakatifu wameteseka sana," aliongeza.

 

4105311

Kishikizo: sistani papa francis
captcha