IQNA

Harakati za Qur'ani Algeria

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya Algeria yaanza

22:34 - December 08, 2022
Habari ID: 3476218
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu na masuala ya Kiislamu ya Algeria imetangaza kuzindua duru ya awali ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani.

Wizara hiyo ilisema katika taarifa siku ya Jumatano kwamba duru ya kwanza ilianza katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Mashindano hayo yanafanyika katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu katika sehemu mbili tofauti kwa wanaume na wanawake, ilisema taarifa hiyo.

Washiriki wanapaswa kuwa na ufasaha katika  mbinu za qiraa za Warsh na Nafi na wawe na uwezo juu wa kuzingatia kanuni Tajweed.

Wizara iliongeza kuwa kikomo cha umri kwa washiriki ni kuanzia miaka 15 hadi 25.

Idara za Awqaf na masuala ya Kiislamu katika miji mikubwa na midogo kote nchini Algeria zinaandaa duru ya awali.

Wale watakaofanya vyema zaidi katika raundi hii watafuzu kwa hatua ya fainali, ambayo imepangwa 2023.

Washindi wakuu watafanikiwa kuingia katika mashindano ya kimataifa ya Algeria ya kuhifadhi Qur'ani na Tajweed.

Algeria ni nchi iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

 

4105477

captcha