IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Rais wa Kyrgyzstan ampongeza mshindi Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani

20:16 - December 02, 2022
Habari ID: 3476184
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Kyrgyzstan, Sadyr Japarov, amekutana na mwakilishi wa nchi hiyo aliyeibuka mshindi wa mashindano ya hivi karibuni ya kimataifa ya Qur'ani nchini Saudi Arabia.

Japarov alimpongeza Mukhamadali Umarov, hafidh wa  Qur'ani Tukufu, kwa kushinda mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu ya Saudi Arabia.

Pia alimtakia Umarov afya njema na mafanikio zaidi.

Umarov  akiwa ameandamana na mwalimu wake Marat Erkulov walimfahamisha Rais Japarov kwamba mashindano hayo ya Qur’ani ya Saudia  ya mwezi uliopita yalikuwa na washiriki 153 kutoka nchi 111.

Umarov mwenye umri wa miaka 24 alisema alijiandaa kwa muda wa miezi mitatu, ambapo alihifadhi aya za za Qur'ani na hatimaye wakati wa mashindano alitambuliwa kuwa ndiye washiriki bora zaidi.

Japarov alimkabidhi Umarov nakala ya maandishi ya Msahafu unaokadiriwa kuandikwa miaka 400 iliyopita.

Kyrgyzstan  au Kirgizia ni nchi ya Asia ya Kati inayopakana na na Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan na China. Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi".

Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti. Karibu asilimia 70 yaa  ya watu wote milioni sita na nusu nchini humo ni Waislamu.

3481491

captcha