IQNA

Msomi wa Kiislamu

Mtarjumi wa Kiarabu-Kiingereza Aisha Bewley aibuka 'Mwanamke Bora wa Mwaka' Mwislamu

21:39 - November 24, 2022
Habari ID: 3476143
TEHRAN (IQNA)- Aisha Bewley, mtarjumi na mfasiri mashuhuri wa Kiarabu-Kiingereza, ametajwa kuwa mwanamke wa Kiislamu wa mwaka katika toleo la 2023 la Muslim 500, chapisho ambalo linawasifu Waislamu wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani.

Bi Bewley, ambaye anajulikana sana kwa kutafsiri fasihi za jadi za Kiislamu katika Kiingereza, amefanya kazi kwa bidii kwa miaka mingi ili kuhakikisha kwamba Waislamu wanaozungumza Kiingereza wanapata fasihi ya Kiislamu iliyoandikwa kwa Kiarabu.

"Aisha Abdurrahman Bewley (aliyezaliwa 1948) ni mmoja wa wafasiri mahiri na waliotabahari duniani wa maandishi ya kale ya Kiislamu kutoka Kiarabu hadi Kiingereza," ilisema ripoti hiyo.

Jarida  la ‘Muslim 500’ liliongeza kuwa tangu kusilimu mwaka 1968, "ametumia miongo mitano iliyopita kujifunza kwa uaminifu mila ya Kiislamu na kufanya maandishi yake muhimu yapatikane kwa Waislamu wanaozungumza Kiingereza duniani kote, wakati mwingine kwa kushirikiana na mumewe, Abdalhaqq Bewley ambaye naye alitarjumi Qur'ani tukufu."

Bi Bewley ameandika na kutafsiri vitabu kadhaa kuhusu Uislamu ili kuiweka wazi dini hii tukufu kwa watu wengi  zaidi kwa sababu hapo awali vitabu hivyo vilikuwa vinapatikana kwa Kiarabu tu.

4102036

captcha