IQNA

Maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana Ubeberu nchini Iran

TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Iran wameshirikiki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu inayosadifiana na leo 4 Novemba, ambapo wamesisitiza udharura kuwepo mapambano endelevu dhidi ya njama za kuzusha fitna, ghasia na fujo.

Miaka 43 iliyopita katika siku hii (Aban 13, 1358, sawa na Novemba 4, 1979), wanachuo wa vyuo vikuu vya Iran waliliteka Pango la Ujasusi la Marekani (Ubalozi) mjini Tehran kulalamikia njama kadhaa wa kadhaa zilizokuwa zikifanywa na Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Tarehe 13 Aban, sawa na Novemba 4 ni kumbukumbu ya matukio matatu muhimu katika vipindi vitatu nyeti na hasasi vya historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Matukio hayo matatu muhimu ya kumbukumbu ni siku aliyobaidishwa na kupelekwa uhamishoni nchini Uturuki Imam Khomeini (MA) tarehe 4 Novemba 1964, siku waliyouliwa wanafunzi na askari wa utawala wa Pahlavi Novemba 4, 1978 na siku ilipofanyika harakati ya kimapinduzi ya kuliteka Pango la Ujasusi la uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran.