IQNA

Wanawake katika Uislamu

Taasisi ya Teknolojia ya Mustafa (SAW) yajadili mustakabali wa wanawake

22:28 - September 16, 2022
Habari ID: 3475793
TEHRAN (IQNA) – Taasisi ya Mustafa(SAW) ya Sayansi na Teknolojia hivi karibuni iliandaa jopo la kisayansi kwa ushirikiano na Jukwaa la Kimataifa la Wanawake katika Sayansi ili kujadili mustakabali endelevu unaojumuisha jinsia kupitia sayansi, teknolojia na uvumbuzi.

Suala kuu lililojadiliwa katika jopo hilo Jumatano 14 Septemba lilikuwa jukumu la jinsia katika kufikia malengo yote ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa. Ana Persic, Mtaalamu wa mipango katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), alizungumza kuhusu usawa wa kijinsia katika UNESCO katika nyanja ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi.

"Sayansi, teknolojia na uvumbuzi vina jukumu muhimu katika kufikia malengo yote ya maendeleo endelevu, na pia usawa wa kijinsia," Parsic alisema.

"Kupunguza ukosefu wa usawa kwa kuvutia wanawake zaidi katika nyanja za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabi kwa kifupu STEM kutasaidia kufikiwa kwa malengo ya SDG," aliongeza.

Zaidi ya hayo, kulingana na ripoti ya Sayansi ya UNESCO, kwa ujumla asilimia 33.3 ya jumla ya watafiti duniani ni wanawake. Akifafanua idadi hii, Persic alisema kuwa nafasi za uongozi miongoni mwa wanawake ni asilimia 12 pekee.

"Maendeleo endelevu yanaweza kupatikana tu wakati wanawake watapata taarifa sawa za kisayansi na taaluma za kisayansi kwa sababu dunia haiwezi kumudu kupuuza uwezo wa kisayansi na akili ya nusu ya wakazi wa dunia," alisisitiza.

Kisha, Jackie Ying mshindi wa Tuzo ya Mustafa(SAW) 2015, alitoa hotuba kuhusu Nanoteknolojia na kuitaja kuwa "zana kuwezesha karne ya 21." Alizungumza kuhusu changamoto kuu za karne ya 21 katika uhandisi zinazoathiri uendelevu, afya,  na furaha ya kuishi. Orzala Nemat kutoka Kitengo cha Utafiti na Tathmini cha Afghanistan, alishughulikia umoja wa wavumbuzi na wanateknolojia wa kike.

Nemat alisema kuwa kwa uvamizi wa vikundi vyenye msimamo mkali nchini Afghanistan  ajenda ya ukoloni dhidi ya nchi hiyo ni mambo ambayo yamewaweka wanawake gizani.

MSTF Holds Panel to Discuss Women’s Role in Sustainable Future  

Kulingana na Nemat, wanaodai kuleta utawala waa Kiislamu nchini wanasimama dhidi ya wanawake kwa njia "isiyo ya Kiislamu" kwa kupiga marufuku elimu ya sekondari kwa wasichana kote Afghanistan.

Hata hivyo, wanawake wa Afghanistan hawajajisalimisha.

Aliangazia takwimu za kike ambazo zimepuuza  na vyombo vya habari vya kawaida. Alimtambulisha Shakardokht Jafari, Mwanafizikia wa Tiba wa Afghanistan ambaye alibuni mbinu ya ufanisi na ya gharama nafuu ya kupima kipimo cha matibabu ya mionzi.

Zaidi ya hayo, Nemat alianzisha Timu ya Roboti ya Wasichana wa Afghanistan, pia inajulikana kama Afghan Dreamers, ambao ni timu ya roboti ya wasichana wote kutoka Herat.

Mzungumzaji mwingine, Rike Yudianti, profesa katika Kituo cha Utafiti cha Nyenzo za Hali ya Juu nchini Indonesia na mmoja wa wageni mashuhuri wa Wiki ya Tuzo ya Mustafa(SAW), alishughulikia ushiriki wa wanawake katika majukwaa ya utafiti na uvumbuzi na haswa mchango wa wanawake wa Indonesia katika sayansi.

Jopo la pili lilifunguliwa na Aini Ideris ambaye alihadhiri kuhusu Uongozi wa Wanawake katika Sayansi akishikilia kwamba "sayansi ina deni kubwa kwa wanawake," Ideris aliwasilisha takwimu za wanawake na waanzilishi katika STEM kuanzia 1300 Kabla  ya Masihi hadi muongo 1960s.

Kisha alirejelea kwa usahihi mitazamo ya kijinsia ambayo inazuia nafasi za wanawake kuchukua majukumu ya uongozi.

Ilkay Erdogan Orhan, mmoja wa wageni mashuhuri wa Mipango ya Mabadilishano ya Sayansi na Teknolojia katika  Taasisi ya Mustafa(SAW) ya Sayansi na Teknolojia, alifungua hotuba yake kwa kushughulikia suala la tofauti ya kijinsia, ambalo aliitaja kama "tatizo kubwa zaidi katika sayansi."

Kwa kuzingatia data ya kukatisha tamaa juu ya idadi ya wanawake wanaojiandikisha katika nyanja za STEM mnamo 2018, Erdogan alisema kuwa wanawake wanahitaji mifano ya kuigwa ambao wanaweza kuhusiana nao.

Erdogan pia alisema kuwa asilimia 33 ya watafiti katika nchi za  Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ni wanawake, lakini katika baadhi ya nchi za eneo hilo, zaidi ya nusu ya watu wazima hawajui kusoma na kuandika na zaidi ya asilimia 70 ya wanawake hawajui kusoma na kuandika.

3480509

captcha