IQNA

Ukombozi wa Palestina

Khalid Mash'al: Wapalestina ni imara na hawataruhusu Msikiti wa Al Aqsa utekwe na Mayahudi

21:17 - May 18, 2022
Habari ID: 3475263
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nje ya nchi amesisitiza kuwa, Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ni eneo la kidini na ni la Kiislamu kikamilifu na kwamba, wananchi wa Palestina hawataruhusu kutekelezwa njama chafu za kuliyahudisha eneo hilo takatifu.

Khalid Mash'al, Kiongozi HAMAS nje ya nchi amebainisha kwamba, wananchi wa Palestina wako imara na katu hawataruhusu Masjidul-Aqsa ifanywe kuwa ni ya Mayahudi iwe ni kwa kuligawa eneo hilo au kulibomoa.

Bwana Mash'al ameeleza kwamba, mipango michafu ya Wazayuni ingalipo hivyo amewatahadharisha wananchi wa Palestina kwamba, vita na makabaliano bado hayajaisha kwani katika siku za usoni inatarajiwa Wazayuni watavamia tena Msikiti wa al-Aqswa katika minasaba siku za usoni.

Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina nje ya nchi ameongeza kuwa, adui Mzayuni anajidanganya kwa kudhani kwamba, kuzuia muqawama wa silaha katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutaandaa uwanja wa kuendelezwa ujenzi wa vitongojii haramu vya walowezi wa Kizayuni na hivyo kutwaa ardhi na kuwa na udhibiti kamili kwa Masjidul-Aqswa.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala haramu wa Israel umeshadidisha njama zake dhidi ya Wapalestina na hasa katika msikiti wa al-Aqsa sambamba na kuongeza kasi ya ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

Hatua hizo zinakwenda sambamba na kuongeza jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina huku Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zikishindwa kuchukukulia hatua utawala huo unaotenda jinai na mauaji kila leo huko Palestina.

/4057897

captcha