IQNA

HAMAS: Utawala wa Kizayuni Lazima Uwajibishwe katika ICC kwa Uhalifu dhidi ya Wapalestina

19:26 - July 30, 2021
Habari ID: 3474141
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesiistiza ulazima wa kuuwajibisha utawala haramu wa Israeli kwa uhalifu wake dhidi ya Wapalestina.

HAMAS imesisitiza ulazima na kuwashtaki viongozi wa utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kufuatia kitendo cha askari wa Israel kumpiga risasi na kumuua kwa kijana Mpalestina katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Msemaji wa Hamas Hazem Qasem alisema hayo katika taarifa kwa vyombo vya habari na kusema mauaji hayo ni "uhalifu kamili wa vita" kwani  Israeli imemuua mtoto wa miaka 12 ambaye alikuwa akipanda gari na baba yake katika Ukingo wa Magharibi Jumatano.

"Kuendelea kwa jeshi la Israel kufanya uhalifu dhidi ya watoto wetu kunaonyesha hisia zake za kila wakati kuwa iko juu y sheria za kimataifa," Qasem alisema.

Msemaji wa Hamas pia alisisitiza kuwa kuzinduliwa kwa operesheni ya mapambano dhidi ya uvamizi wa Israeli katika Ukingo wa Magharibi ndio njia pekee ya kukabiliana na uhalifu wa utawala huo ghasibu.

Upigaji risasi mbaya wa kijana huyo wa Kipalestina ulifanyika Jumatano karibu na mlango wa mji wa Beit Ummar, kaskazini mwa mji wa al-Khalil wa Ukingo wa Magharibi.

Wizara ya Afya ya Palestina ilisema Mohammad Mouayyad Allamy alipigwa risasi kifuani na kuvuja damu katika mapafu yake wakati majeshi ya Israeli yalipofyatua risasi gari bila sababu, na kuongeza kuwa kijana huyo alihamishwa na madaktari wakiwa katika hali mbaya kwenda Hospitali ya al-Ahli, lakini baadaye alikufa kwa majeraha yake.

Mohammad alikuwa kijana wa pili wa Kipalestina kufa kwa majeraha yaliyotokana na moto wa Israeli hivi karibuni.

Vikosi vya Israeli vilivamia mnamo Julai 24 mji wa Beita, kusini mwa Nablus, na kumuua kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 17 kwenye maandamano ya makazi haramu katika Ukingo wa Magharibi.

3475367

captcha