IQNA

Haram ya Imam Jawad AS, Kadhimiya nchini Iraq

19:00 - July 11, 2021
Habari ID: 3474090
TEHRAN (IQNA)- Leo ni Jumapili tarehe 30 Dhulqaada 1442 Hijria Qamaria inayosadifiana na tarehe 11 Julai 2021 ni siku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Muhammad Taqi AS mmoja kati ya wajukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW.

Mtukufu huyo alipewa jina la 'Jawad' likiwa na maana ya mtu mkarimu sana kutokana na ukarimu wake mkubwa. Imam Jawad alizaliwa katika mwezi wa Ramadhani mwaka 195 Hijria na kuongoza Umma wa Kiislamu baada ya kuuawa shahidi baba yake, Imam Ridha AS. Aliuawa shahidi akiwa na umri wa miaka 25 na amezikwa pembizoni mwa babu yake, Imam Musa Kadhim AS katika eneo la Kadhimiya kaskazini mwa Baghdad.

 
 
captcha