IQNA

Taj Mahal lafutwa katika kitabu cha utalii India kwa sababu ni turathi ya Kiislamu

11:14 - October 10, 2017
Habari ID: 3471210
TEHRAN (IQNA)-Jengo la Taj Mahal nchini India, moja kati ya Maajabu Saba ya Dunia, na ambalo huwavutia watalii wasiopungua milioni sita kwa mwaka limeondolewa katika orodha ya vivutio vya kitalii kwa sababu ni turathi ya Kiislamu.

Jengo hilo lenye usanifu majengo mahiri wa Kiislamu huwavutia watalii kuliko eneo lolote India, lakini sasa inaonekana serikali ya jimbo la Uttar Pradesh yenye misimamo mikali ya Kihindu inaonekana kutofurahishwa na Taj Mahal.

Hii ni katika hali ambayo jengo hilo la aina yake na linalosimulia historia ya ushawishi wa Waislamu india liko katika orodha ya UNESCO ya turathi za dunia. Jengo hilo ambalo linatazamwa na wengi duniani kama "Nembo ya Mapenzi" sasa limeondolewa katika kitabu cha utalii cha serikali ya jimbo la Uttar Pradesh.

Sohail Hashmir, mwandishi na maaalamu ywa turathi anakilamulu cha tawala India cha Bharatiya Janata (BJP), chenye misimamo mikali ya Kihindu, kuwa kimeingiza siasa katika suala la Taj Mahal.

"BJP kimeingia madarakani kwa msingi Wahindi ni wale tu wanaofungamana na itikadi ya Uhindu. Kwa msingi huo Taj Mahal haipo katika mtazamo wao wa utamaduni," ameiambia televisheni ya Al Jazeera.

Taj Mahal ni jengo zuri la kaburi lenye umbo la msikiti mjini Agra nchini India na huhesabiwa kati ya majengo mazuri duniani.

Taj Mahal ilijengwa 1631 - 1648 Miladia kwa amri ya Shah Jahan aliyekuwa mtawala wa nasaba ya Moghul aliyetaka kumkumbuka mke wake mpendwa 1631 Mumtaz Mahal. Shah Jahan aliwaajiri mafundi 20,000 kutoka Asia ya Kusini na Asia ya Kati walioongozwa na Mwajemi Ali Fazal. Msanifu huyu aliunganisha sifa za ujenzi wa Uajemi na Uhindi.

Jengo liko hatarini kutokana na hewa chafu. Magari hayaruhusiwi kukaribia jengo katika duara ya kilomita 2. Hata hivyo gesi chafu na mvua asidi zinaendelea kula mawe yake.

3650874

captcha